Native Bible

Job 18:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?

Job 18:4 in English

Job 18:4 · Berean Standard Bible

You who tear yourself in anger— should the earth be forsaken on your account, or the rocks be moved from their place?

Context

2“Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea. 3Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako? 4Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake? 5“Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika. 6Mwanga hemani mwake umekuwa giza; taa iliyo karibu naye imezimika.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.