Ayubu 15:29
Job 15:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu, wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi.
Job 15:29 in English
Job 15:29 · Berean Standard Bible
He will no longer be rich; his wealth will not endure. His possessions will not overspread the land.
Context
27“Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unene
na kiuno chake kimevimba kwa kunenepa, 28ataishi katika miji ya magofu,
na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote,
nyumba zinazokuwa vifusi. 29Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu,
wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi. 30Hatatoka gizani;
mwali wa moto utanyausha machipukizi yake,
nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali. 31Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili,
kwa kuwa hatapata malipo yoyote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.