Ayubu 14:13
Job 14:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Laiti kama ungenificha kaburini,* na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka!
Job 14:13 in English
Job 14:13 · Berean Standard Bible
If only You would hide me in Sheol and conceal me until Your anger has passed! If only You would appoint a time for me and then remember me!
Context
11Kama vile maji yatowekavyo katika bahari,
au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu, 12ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke;
hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena,
wanadamu hawataamka au kuamshwa
kutoka kwenye usingizi wao. 13“Laiti kama ungenificha kaburini,*
na kunisitiri hadi hasira yako ipite!
Laiti ungeniwekea wakati,
na kisha ukanikumbuka! 14Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena?
Siku zote za kazi zangu ngumu
nitangojea kufanywa upya kwangu. 15Utaniita nami nitakuitika;
utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.