Native Bible

Job 10:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.

Job 10:2 in English

Job 10:2 · Berean Standard Bible

I will say to God: Do not condemn me! Let me know why You prosecute me.

Context

1“Nayachukia sana haya maisha yangu; kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu. 2Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu. 3Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu? 4Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.