Ayubu 10:17
Job 10:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira yako juu yangu; nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine.
Job 10:17 in English
Job 10:17 · Berean Standard Bible
You produce new witnesses against me and multiply Your anger toward me. Hardships assault me in wave after wave.
Context
15Kama nina hatia, ole wangu!
Hata kama ningekuwa sina hatia,
siwezi kukiinua kichwa changu,
kwa kuwa nimejawa na aibu,
na kuzama katika mateso yangu. 16Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba,
na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu. 17Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu
na kuzidisha hasira yako juu yangu;
nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine. 18“Kwa nini basi ulinitoa tumboni?
Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona. 19Laiti nisingekuwako kamwe,
au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja
kutoka tumboni kwenda kaburini!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.