Yohana 9:23
John 9:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Muulizeni.”
John 9:23 in English
John 9:23 · Berean Standard Bible
That was why his parents said, “He is old enough. Ask him.”
Context
21Lakini sisi hatujui ni kwa jinsi gani kwamba sasa anaona, wala hatujui ni nani aliyemfungua macho yake. Muulizeni, yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.” 22Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa Wayahudi kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Yesu kuwa ndiye Kristo* atafukuzwa kutoka sinagogi. 23Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Muulizeni.” 24Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.” 25Akawajibu, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi. Lakini jambo moja ninalojua, nilikuwa kipofu na sasa ninaona.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.