Native Bible

John 8:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote.

John 8:3 in English

John 8:3 · Berean Standard Bible

The scribes and Pharisees, however, brought to Him a woman caught in adultery. They made her stand before them

Context

1Lakini Yesu akaenda katika Mlima wa Mizeituni. 2Alfajiri na mapema Yesu akaja tena Hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha. 3Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote. 4Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. 5Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.