Native Bible

John 6:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati huu wote?”

John 6:9 in English

John 6:9 · Berean Standard Bible

“Here is a boy with five barley loaves and two small fish. But what difference will these make among so many?”

Context

7Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili,* hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.” 8Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia, 9“Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati huu wote?” 10Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi. Palikuwa na wanaume wapatao 5,000. 11Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.