Yohana 6:21
John 6:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.
John 6:21 in English
John 6:21 · Berean Standard Bible
Then they were willing to take Him into the boat, and at once the boat reached the shore where they were heading.
Context
19Wanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne,* walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana. 20Lakini Yesu akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.” 21Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda. 22Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ngʼambo waliona kwamba palikuwepo na mashua moja tu na kwamba Yesu hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao. 23Lakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia zikafika karibu na mahali pale walipokula mikate baada ya Bwana kumshukuru Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.