Yohana 4:8
John 4:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)
John 4:8 in English
John 4:8 · Berean Standard Bible
(His disciples had gone into the town to buy food.)
Context
6Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. 7Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, “Naomba maji ninywe.” 8(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.) 9Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.) 10Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.