Yohana 4:48
John 4:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”
John 4:48 in English
John 4:48 · Berean Standard Bible
Jesus said to him, “Unless you people see signs and wonders, you will never believe.”
Context
46Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwepo na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. 47Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa. 48Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.” 49Yule afisa wa mfalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.” 50Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.”
Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.