Yohana 4:50
John 4:50 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.” Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake.
John 4:50 in English
John 4:50 · Berean Standard Bible
“Go,” said Jesus. “Your son will live.” The man took Jesus at His word and departed.
Context
48Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.” 49Yule afisa wa mfalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.” 50Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.”
Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake. 51Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. 52Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.