Native Bible

John 3:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake.

John 3:32 in English

John 3:32 · Berean Standard Bible

He testifies to what He has seen and heard, yet no one accepts His testimony.

Context

30Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.” 31“Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. 32Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake. 33Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. 34Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.