Yohana 21:9
John 21:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate.
John 21:9 in English
John 21:9 · Berean Standard Bible
When they landed, they saw a charcoal fire there with fish on it, and some bread.
Context
7Yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini. 8Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 200* 9Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate. 10Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.” 11Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.