Native Bible

John 21:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.”

John 21:10 in English

John 21:10 · Berean Standard Bible

Jesus told them, “Bring some of the fish you have just caught.”

Context

8Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 200* 9Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate. 10Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.” 11Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12Yesu akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanafunzi aliyethubutu kumuuliza, “Wewe ni nani?” Kwa sababu walijua ya kuwa ni Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.