Yohana 17:14
John 17:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu.
John 17:14 in English
John 17:14 · Berean Standard Bible
I have given them Your word and the world has hated them; for they are not of the world, just as I am not of the world.
Context
12Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia. 13“Lakini sasa naja kwako, nami ninasema mambo haya wakati bado nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kamili ndani yao. 14Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu. 15Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu. 16Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.