Native Bible

John 16:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi.

John 16:3 in English

John 16:3 · Berean Standard Bible

They will do these things because they have not known the Father or Me.

Context

1“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. 2Watawatenga na masinagogi. Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu. 3Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi. 4Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi. 5“Sasa mimi ninakwenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unakwenda wapi?’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.