Native Bible

John 15:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi.

John 15:3 in English

John 15:3 · Berean Standard Bible

You are already clean because of the word I have spoken to you.

Context

1“Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 2Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. 3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi. 4Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda. 5“Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.