Yohana 12:11
John 12:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Yesu na kumwamini.
John 12:11 in English
John 12:11 · Berean Standard Bible
for on account of him many of the Jews were deserting them and believing in Jesus.
Context
9Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Yesu alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Yesu, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua. 10Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 11kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake Wayahudi wengi walikuwa wanamwendea Yesu na kumwamini. 12Siku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. 13Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema,
“Hosana!”*
“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
“Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.