Yohana 10:14
John 10:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua.
John 10:14 in English
John 10:14 · Berean Standard Bible
I am the good shepherd. I know My sheep and My sheep know Me,
Context
12Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Amwonapo mbwa mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya. 13Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo. 14“Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua. 15Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.