Yohana 1:38
John 1:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?”
John 1:38 in English
John 1:38 · Berean Standard Bible
Jesus turned and saw them following. “What do you want?” He asked. They said to Him, “Rabbi” (which means Teacher), “where are You staying?”
Context
36Alipomwona Yesu akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!” 37Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 38Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?”
Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?” 39Yesu akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!”
Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi. 40Andrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye alimfuata Yesu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.