Yeremia 8:5
Jeremiah 8:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa nini basi watu hawa walipotea? Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara? Wanangʼangʼania udanganyifu na wanakataa kurudi.
Jeremiah 8:5 in English
Jeremiah 8:5 · Berean Standard Bible
Why then have these people turned away? Why does Jerusalem always turn away? They cling to deceit; they refuse to return.
Context
3Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’ 4“Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana:
“ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki?
Je, mtu anapopotea harudi? 5Kwa nini basi watu hawa walipotea?
Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara?
Wanangʼangʼania udanganyifu
na wanakataa kurudi. 6Nimewasikiliza kwa makini,
lakini hawataki kusema lililo sawa.
Hakuna anayetubia makosa yake
akisema, “Nimefanya nini?”
Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe
kama farasi anayekwenda vitani. 7Hata korongo aliyeko angani
anayajua majira yake yaliyoamriwa,
nao njiwa, mbayuwayu na koikoi
hufuata majira yao ya kurudi.
Lakini watu wangu hawajui
Bwana anachotaka kwao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.