Yeremia 6:25
Jeremiah 6:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usitoke kwenda mashambani au kutembea barabarani, kwa kuwa adui ana upanga, na kuna vitisho kila upande.
Jeremiah 6:25 in English
Jeremiah 6:25 · Berean Standard Bible
Do not go out to the fields; do not walk the road. For the enemy has a sword; terror is on every side.
Context
23Wamejifunga pinde na mkuki,
ni wakatili na hawana huruma.
Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma
wanapoendesha farasi zao.
Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita
ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.” 24Tumesikia taarifa zao,
nayo mikono yetu imelegea.
Uchungu umetushika,
maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 25Usitoke kwenda mashambani
au kutembea barabarani,
kwa kuwa adui ana upanga,
na kuna vitisho kila upande. 26Enyi watu wangu, vaeni magunia
mjivingirishe kwenye majivu,
ombolezeni kwa kilio cha uchungu
kama amliliaye mwana pekee,
kwa maana ghafula
mharabu atatujia. 27“Nimekufanya wewe kuwa kitu cha kujaribu chuma,
nao watu wangu kama mawe yenye madini,
ili upate kuzijua na kuzijaribu njia zao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.