Yeremia 6:19
Jeremiah 6:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sikia, ee nchi: Ninaleta maafa juu ya watu hawa, matunda ya mipango yao, kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu na wameikataa sheria yangu.
Jeremiah 6:19 in English
Jeremiah 6:19 · Berean Standard Bible
Hear, O earth! I am bringing disaster on this people, the fruit of their own schemes, because they have paid no attention to My word and have rejected My instruction.
Context
17Niliweka walinzi juu yenu na kusema,
‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’
Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’ 18Kwa hiyo sikilizeni, enyi mataifa,
angalieni, enyi mashahidi,
lile litakalowatokea. 19Sikia, ee nchi:
Ninaleta maafa juu ya watu hawa,
matunda ya mipango yao,
kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu
na wameikataa sheria yangu. 20Unanifaa nini uvumba kutoka Sheba,
au udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?
Sadaka zako za kuteketezwa hazikubaliki,
dhabihu zako hazinifurahishi mimi.” 21Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Bwana:
“Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa.
Baba na wana wao watajikwaa juu yake,
majirani na marafiki wataangamia.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.