Yeremia 51:6
Jeremiah 51:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kimbieni kutoka Babeli! Okoeni maisha yenu! Msiangamizwe kwa sababu ya dhambi zake. Ni wakati wa kisasi cha Bwana, atamlipa kile anachostahili.
Jeremiah 51:6 in English
Jeremiah 51:6 · Berean Standard Bible
Flee from Babylon! Escape with your lives! Do not be destroyed in her punishment. For this is the time of the LORD’s vengeance; He will pay her what she deserves.
Context
4Wataanguka waliouawa katika Babeli,
wakiwa na majeraha ya kutisha barabarani zake. 5Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwa
na Mungu wao, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
ingawa nchi yao imejaa uovu
mbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 6“Kimbieni kutoka Babeli!
Okoeni maisha yenu!
Msiangamizwe kwa sababu ya dhambi zake.
Ni wakati wa kisasi cha Bwana,
atamlipa kile anachostahili. 7Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa Bwana;
aliufanya ulimwengu wote ulewe.
Mataifa walikunywa mvinyo wake;
kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu. 8Babeli ataanguka ghafula na kuvunjika.
Mwombolezeni!
Tafuteni zeri ya kutuliza maumivu yake,
labda anaweza kupona.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.