Yeremia 51:57
Jeremiah 51:57 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Jeremiah 51:57 in English
Jeremiah 51:57 · Berean Standard Bible
I will make her princes and wise men drunk, along with her governors, officials, and warriors. Then they will fall asleep forever and not wake up,” declares the King, whose name is the LORD of Hosts.
Context
55Bwana ataiangamiza Babeli,
atanyamazisha makelele ya kishindo chake.
Mawimbi ya adui yatanguruma kama maji makuu,
ngurumo ya sauti zao itavuma. 56Mharabu atakuja dhidi ya Babeli,
mashujaa wake watakamatwa,
nazo pinde zao zitavunjwa.
Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa kisasi,
yeye atalipiza kikamilifu. 57Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe,
watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao;
watalala milele na hawataamka,”
asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote. 58Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa,
na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto;
mataifa yanajichosha bure,
taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.” 59Huu ndio ujumbe Yeremia aliompa afisa Seraya mwana wa Neria mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.