Yeremia 51:33
Jeremiah 51:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria wakati inapokanyagwa; wakati wa kumvuna utakuja upesi.”
Jeremiah 51:33 in English
Jeremiah 51:33 · Berean Standard Bible
For this is what the LORD of Hosts, the God of Israel, says: “The Daughter of Babylon is like a threshing floor at the time it is trampled. In just a little while her harvest time will come.”
Context
31Tarishi mmoja humfuata mwingine,
na mjumbe humfuata mjumbe,
kumtangazia mfalme wa Babeli
kwamba mji wake wote umetekwa, 32Vivuko vya mito vimekamatwa,
mabwawa yenye mafunjo yametiwa moto,
nao askari wameingiwa na hofu kuu.” 33Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:
“Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria
wakati inapokanyagwa;
wakati wa kumvuna utakuja upesi.” 34“Nebukadneza mfalme wa Babeli ametula,
ametufanya tuchangayikiwe,
ametufanya tuwe gudulia tupu.
Kama nyoka ametumeza
na kujaza tumbo lake kwa vyakula vyetu vizuri,
kisha akatutapika. 35Jeuri iliyofanyiwa miili yetu* na iwe juu ya Babeli,”
ndivyo wasemavyo wakaao Sayuni.
“Damu yetu na iwe juu ya wale waishio Babeli,”
asema Yerusalemu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.