Yeremia 51:29
Jeremiah 51:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nchi inatetemeka na kugaagaa, kwa kuwa makusudi ya Bwana dhidi ya Babeli yanasimama: yaani, kuangamiza nchi ya Babeli ili pasiwe na yeyote atakayeishi humo.
Jeremiah 51:29 in English
Jeremiah 51:29 · Berean Standard Bible
The earth quakes and writhes because the LORD’s intentions against Babylon stand: to make the land of Babylon a desolation, without inhabitant.
Context
27“Twekeni bendera katika nchi!
Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa!
Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,
iteni falme hizi dhidi yake:
Ararati, Mini na Ashkenazi.
Wekeni jemadari dhidi yake,
pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige. 28Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,
wafalme wa Wamedi,
watawala wao na maafisa wao wote,
pamoja na nchi zote wanazotawala. 29Nchi inatetemeka na kugaagaa,
kwa kuwa makusudi ya Bwana dhidi ya Babeli yanasimama:
yaani, kuangamiza nchi ya Babeli
ili pasiwe na yeyote atakayeishi humo. 30Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana,
wamebaki katika ngome zao.
Nguvu zao zimekwisha,
wamekuwa kama wanawake.
Makazi yake yameteketezwa kwa moto,
makomeo ya malango yake yamevunjika. 31Tarishi mmoja humfuata mwingine,
na mjumbe humfuata mjumbe,
kumtangazia mfalme wa Babeli
kwamba mji wake wote umetekwa,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.