Yeremia 51:26
Jeremiah 51:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakuna jiwe litakalochukuliwa kutoka kwako kwa ajili ya kufanywa jiwe la pembeni, wala jiwe lolote kwa ajili ya msingi, kwa maana utakuwa ukiwa milele,” asema Bwana.
Jeremiah 51:26 in English
Jeremiah 51:26 · Berean Standard Bible
No one shall retrieve from you a cornerstone or a foundation stone, because you will become desolate forever,” declares the LORD.
Context
24“Mbele ya macho yako nitamlipiza Babeli na wote waishio Ukaldayo kwa ajili ya makosa yote waliyofanya katika Sayuni,” asema Bwana. 25“Mimi niko kinyume nawe, ee mlima unaoharibu,
wewe uangamizaye dunia yote,”
asema Bwana.
“Nitanyoosha mkono wangu dhidi yako,
nikuvingirishe kutoka kwenye kilele cha mwamba,
na kukufanya mlima ulioteketezwa kwa moto. 26Hakuna jiwe litakalochukuliwa kutoka kwako
kwa ajili ya kufanywa jiwe la pembeni,
wala jiwe lolote kwa ajili ya msingi,
kwa maana utakuwa ukiwa milele,”
asema Bwana. 27“Twekeni bendera katika nchi!
Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa!
Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,
iteni falme hizi dhidi yake:
Ararati, Mini na Ashkenazi.
Wekeni jemadari dhidi yake,
pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige. 28Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake,
wafalme wa Wamedi,
watawala wao na maafisa wao wote,
pamoja na nchi zote wanazotawala.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.