Yeremia 51:18
Jeremiah 51:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha, hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia.
Jeremiah 51:18 in English
Jeremiah 51:18 · Berean Standard Bible
They are worthless, a work to be mocked. In the time of their punishment they will perish.
Context
16Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma,
huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia.
Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua,
naye huuleta upepo kutoka ghala zake. 17“Kila mtu ni mjinga na hana maarifa;
kila sonara ameaibishwa na sanamu zake.
Vinyago vyake ni vya udanganyifu,
havina pumzi ndani yavyo. 18Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha,
hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia. 19Yeye Aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo,
kwani ndiye Muumba wa vitu vyote,
pamoja na kabila la urithi wake:
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. 20“Wewe ndiwe rungu langu la vita,
silaha yangu ya vita:
kwa wewe navunjavunja mataifa,
kwa wewe naangamiza falme,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.