Yeremia 51:13
Jeremiah 51:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wewe uishiye kando ya maji mengi na uliye na wingi wa hazina, mwisho wako umekuja, wakati wako wa kukatiliwa mbali.
Jeremiah 51:13 in English
Jeremiah 51:13 · Berean Standard Bible
You who dwell by many waters, rich in treasures, your end has come; the thread of your life is cut.
Context
11“Noeni mishale,
chukueni ngao!
Bwana amewaamsha wafalme wa Wamedi,
kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli.
Bwana atalipiza kisasi,
kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. 12Twekeni bendera juu ya kuta za Babeli!
Imarisheni ulinzi,
wekeni walinzi,
andaeni waviziao!
Bwana atatimiza kusudi lake,
amri yake juu ya watu wa Babeli. 13Wewe uishiye kando ya maji mengi
na uliye na wingi wa hazina,
mwisho wako umekuja,
wakati wako wa kukatiliwa mbali. 14Bwana Mwenye Nguvu Zote
ameapa kwa nafsi yake mwenyewe:
‘Hakika nitakujaza na watu, kama kundi la nzige,
nao watapiga kelele za ushindi juu yako.’ 15“Aliiumba dunia kwa uweza wake;
akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake
na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.