Yeremia 50:11
Jeremiah 50:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa sababu hushangilia na kufurahi, wewe utekaye urithi wangu, kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka, na kulia kama farasi dume,
Jeremiah 50:11 in English
Jeremiah 50:11 · Berean Standard Bible
“Because you rejoice, because you sing in triumph— you who plunder My inheritance— because you frolic like a heifer treading grain and neigh like stallions,
Context
9Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli
muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini.
Watashika nafasi zao dhidi yake,
naye kutokea kaskazini atatekwa.
Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari,
ambao hawawezi kurudi mikono mitupu. 10Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara;
wote wamtekao nyara watapata za kutosha,”
asema Bwana. 11“Kwa sababu hushangilia na kufurahi,
wewe utekaye urithi wangu,
kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka,
na kulia kama farasi dume, 12mama yako ataaibika mno,
yeye aliyekuzaa atatahayari.
Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote,
atakuwa nyika, nchi kame na jangwa. 13Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu,
lakini ataachwa ukiwa kabisa.
Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki
kwa sababu ya majeraha yake yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.