Yeremia 5:7
Jeremiah 5:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa nini niwasamehe? Watoto wenu wameniacha na kuapa kwa miungu ambayo si miungu. Niliwapatia mahitaji yao yote, lakini bado wamefanya uzinzi na kusongana katika nyumba za makahaba.
Jeremiah 5:7 in English
Jeremiah 5:7 · Berean Standard Bible
“Why should I forgive you? Your children have forsaken Me and sworn by gods that are not gods. I satisfied their needs, yet they committed adultery and assembled at the houses of prostitutes.
Context
5Kwa hiyo nitakwenda kwa viongozi
na kuzungumza nao,
hakika wao wanaijua njia ya Bwana,
sheria ya Mungu wao.”
Lakini kwa nia moja nao pia walikuwa wameivunja nira
na kuvivunja vifungo. 6Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia,
mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza,
chui atawavizia karibu na miji yao,
ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje,
kwa maana maasi yao ni makubwa,
na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi. 7“Kwa nini niwasamehe?
Watoto wenu wameniacha na kuapa kwa miungu ambayo si miungu.
Niliwapatia mahitaji yao yote,
lakini bado wamefanya uzinzi na kusongana katika nyumba za makahaba. 8Wamelishwa vizuri, kama farasi waume wenye tamaa nyingi,
kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine. 9Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”
asema Bwana.
“Je, nisijilipizie kisasi
juu ya taifa kama hili?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.