Yeremia 5:2
Jeremiah 5:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ingawa wanasema, ‘Kwa hakika kama Bwana aishivyo,’ bado wanaapa kwa uongo.”
Jeremiah 5:2 in English
Jeremiah 5:2 · Berean Standard Bible
Although they say, ‘As surely as the LORD lives,’ they are swearing falsely.”
Context
1“Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu,
tazameni pande zote na mtafakari,
tafuteni katika viwanja vyake.
Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu
atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli,
nitausamehe mji huu. 2Ingawa wanasema, ‘Kwa hakika kama Bwana aishivyo,’
bado wanaapa kwa uongo.” 3Ee Bwana, je, macho yako hayaitafuti kweli?
Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu,
uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo.
Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe
nao walikataa kutubu. 4Ndipo nikasema, “Hawa ni maskini tu;
wao ni wapumbavu,
kwa maana hawaijui njia ya Bwana,
sheria ya Mungu wao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.