Yeremia 5:16
Jeremiah 5:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Podo zao ni kama kaburi lililo wazi, wote ni mashujaa hodari wa vita.
Jeremiah 5:16 in English
Jeremiah 5:16 · Berean Standard Bible
Their quivers are like open graves; they are all mighty men.
Context
14Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote:
“Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya,
nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto,
na watu hawa wawe kuni
zinazoliwa na huo moto. 15Ee nyumba ya Israeli,” asema Bwana,
“Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako,
taifa la kale na linaloendelea kudumu,
taifa ambalo lugha yao huijui,
wala msemo wao huwezi kuuelewa. 16Podo zao ni kama kaburi lililo wazi,
wote ni mashujaa hodari wa vita. 17Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu,
wataangamiza wana wenu na mabinti zenu;
wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe,
wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu.
Kwa upanga wataangamiza
miji yenye maboma mliyoitumainia. 18“Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.