Yeremia 49:1
Jeremiah 49:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuhusu Waamoni: Hili ndilo asemalo Bwana: “Je, Israeli hana wana? Je, hana warithi? Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi? Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake?
Jeremiah 49:1 in English
Jeremiah 49:1 · Berean Standard Bible
Concerning the Ammonites, this is what the LORD says: “Has Israel no sons? Is he without heir? Why then has Milcom * taken possession of Gad? Why have his people settled in their cities?
Context
1Kuhusu Waamoni:
Hili ndilo asemalo Bwana:
“Je, Israeli hana wana?
Je, hana warithi?
Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi?
Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake? 2Lakini siku zinakuja,”
asema Bwana,
“nitakapopiga kelele ya vita
dhidi ya Raba mji wa Waamoni;
utakuwa kilima cha magofu,
navyo vijiji vinavyouzunguka
vitateketezwa kwa moto.
Kisha Israeli atawafukuza
wale waliomfukuza,”
asema Bwana. 3“Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa!
Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba!
Vaeni nguo za gunia na kuomboleza,
kimbieni hapa na pale ndani ya kuta,
kwa kuwa Moleki atakwenda uhamishoni,
yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.