Yeremia 48:46
Jeremiah 48:46 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole wako, ee Moabu! Watu wa Kemoshi wameangamizwa; wana wako wamepelekwa uhamishoni na binti zako wamechukuliwa mateka.
Jeremiah 48:46 in English
Jeremiah 48:46 · Berean Standard Bible
Woe to you, O Moab! The people of Chemosh have perished; for your sons have been taken into exile and your daughters have gone into captivity.
Context
44“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu
ataanguka ndani ya shimo,
yeyote atakayepanda kutoka shimoni,
atanaswa katika mtego,
kwa sababu nitaletea Moabu
mwaka wa adhabu yake,”
asema Bwana. 45“Katika kivuli cha Heshboni,
wakimbizi wamesimama pasipo msaada,
kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni,
mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni;
unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu,
mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele. 46Ole wako, ee Moabu!
Watu wa Kemoshi wameangamizwa;
wana wako wamepelekwa uhamishoni
na binti zako wamechukuliwa mateka. 47“Lakini nitarudisha mateka wa Moabu,
katika siku zijazo,”
asema Bwana.
Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.