Yeremia 48:37
Jeremiah 48:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila kichwa kimenyolewa na kila mwenye ndevu zimekatwa; kila mkono umekatwa na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia.
Jeremiah 48:37 in English
Jeremiah 48:37 · Berean Standard Bible
For every head is shaved and every beard is clipped; on every hand is a gash, and around every waist is sackcloth.
Context
35Nitakomesha wale wote katika Moabu
watoao sadaka mahali pa juu,
na kufukiza uvumba kwa miungu yao,”
asema Bwana. 36“Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi;
unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.
Utajiri waliojipatia umetoweka. 37Kila kichwa kimenyolewa
na kila mwenye ndevu zimekatwa;
kila mkono umekatwa
na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia. 38Juu ya mapaa yote katika Moabu
na katika viwanja
hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo,
kwa kuwa nimemvunja Moabu
kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,”
asema Bwana. 39“Tazama jinsi alivyovunjikavunjika!
Jinsi wanavyolia kwa huzuni!
Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu!
Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa,
kitu cha kutisha kwa wale wote
wanaomzunguka.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.