Native Bible

Jeremiah 48:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitakomesha wale wote katika Moabu watoao sadaka mahali pa juu, na kufukiza uvumba kwa miungu yao,” asema Bwana.

Jeremiah 48:35 in English

Jeremiah 48:35 · Berean Standard Bible

In Moab, declares the LORD, I will bring an end to those who make offerings on the high places and burn incense to their gods.

Context

33Shangwe na furaha vimetoweka kutoka bustani na mashamba ya Moabu. Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo; hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe. Ingawa kuna kelele, sio kelele za shangwe. 34“Sauti ya kilio chao inapanda kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi, kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya, kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka. 35Nitakomesha wale wote katika Moabu watoao sadaka mahali pa juu, na kufukiza uvumba kwa miungu yao,” asema Bwana. 36“Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi; unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. Utajiri waliojipatia umetoweka. 37Kila kichwa kimenyolewa na kila mwenye ndevu zimekatwa; kila mkono umekatwa na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.