Yeremia 46:7
Jeremiah 46:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili, kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi?
Jeremiah 46:7 in English
Jeremiah 46:7 · Berean Standard Bible
Who is this, rising like the Nile, like rivers whose waters churn?
Context
5Je, ninaona nini?
Wametiwa hofu,
wanarudi nyuma,
askari wao wameshindwa.
Wanakimbia kwa haraka
pasipo kutazama nyuma,
tena kuna hofu kuu kila upande,”
asema Bwana. 6Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia,
wala wenye nguvu hawawezi kutoroka.
Kaskazini, kando ya Mto Frati,
wanajikwaa na kuanguka. 7“Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili,
kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi? 8Misri hujiinua kama Mto Naili,
kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi.
Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia,
nitaiangamiza miji na watu wake.’ 9Songeni mbele, enyi farasi!
Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi,
Endeleeni mbele, enyi mashujaa:
watu wa Kushi* na Putu* wachukuao ngao,
watu wa Ludi* wavutao upinde.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.