Yeremia 46:3
Jeremiah 46:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo, mtoke kwa ajili ya vita!
Jeremiah 46:3 in English
Jeremiah 46:3 · Berean Standard Bible
“Deploy your shields, small and large; advance for battle!
Context
1Hili ni neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa: 2Kuhusu Misri:
Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: 3“Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo,
mtoke kwa ajili ya vita! 4Fungieni farasi lijamu,
pandeni farasi!
Shikeni nafasi zenu
mkiwa mmevaa chapeo!
Isugueni mikuki yenu,
vaeni dirii vifuani! 5Je, ninaona nini?
Wametiwa hofu,
wanarudi nyuma,
askari wao wameshindwa.
Wanakimbia kwa haraka
pasipo kutazama nyuma,
tena kuna hofu kuu kila upande,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.