Yeremia 46:20
Jeremiah 46:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Misri ni mtamba mzuri, lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini.
Jeremiah 46:20 in English
Jeremiah 46:20 · Berean Standard Bible
Egypt is a beautiful heifer, but a gadfly from the north is coming against her.
Context
18“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,
ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote,
“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima,
kama Karmeli kando ya bahari. 19Funga mizigo yako kwenda uhamishoni,
wewe ukaaye Misri,
kwa kuwa Memfisi utaangamizwa
na kuwa magofu pasipo mkazi. 20“Misri ni mtamba mzuri,
lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini. 21Askari wake waliokodiwa katika safu zake
wako kama ndama walionenepeshwa.
Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,
hawataweza kuhimili vita,
kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,
wakati wao wa kuadhibiwa. 22Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia
kadiri adui anavyowasogelea na majeshi,
watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,
kama watu wakatao miti.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.