Native Bible

Jeremiah 39:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Mchukue umtunze. Usimdhuru, lakini umfanyie chochote anachotaka.”

Jeremiah 39:12 in English

Jeremiah 39:12 · Berean Standard Bible

“Take him, look after him, and do not let any harm come to him; do for him whatever he says.”

Context

10Lakini Nebuzaradani kiongozi wa walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine. 11Basi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa maagizo kuhusu Yeremia kupitia Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme akisema: 12“Mchukue umtunze. Usimdhuru, lakini umfanyie chochote anachotaka.” 13Basi Nebuzaradani kiongozi wa walinzi, Nebushazbani afisa mkuu, Nergal-Shareza afisa wa cheo cha juu, na maafisa wengine wote wa mfalme wa Babeli 14wakatuma watu kumwondoa Yeremia kutoka ua wa walinzi. Wakamkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ili amrudishe nyumbani kwake. Kwa hiyo akabaki miongoni mwa watu wake mwenyewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.