Yeremia 31:36
Jeremiah 31:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,” asema Bwana, “ndipo wazao wa Israeli watakoma kuwa taifa mbele yangu daima.”
Jeremiah 31:36 in English
Jeremiah 31:36 · Berean Standard Bible
“Only if this fixed order departed from My presence, declares the LORD, would Israel’s descendants ever cease to be a nation before Me.”
Context
34Mtu hatamfundisha tena jirani yake,
wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’
kwa sababu wote watanijua mimi,
tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,”
asema Bwana.
“Kwa sababu nitasamehe uovu wao,
wala sitazikumbuka dhambi zao tena.” 35Hili ndilo asemalo Bwana,
yeye aliyeweka jua
liwake mchana,
yeye anayeamuru mwezi na nyota
kungʼaa usiku,
yeye aichafuaye bahari
ili mawimbi yake yangurume;
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake: 36“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,”
asema Bwana,
“ndipo wazao wa Israeli watakoma
kuwa taifa mbele yangu daima.” 37Hili ndilo asemalo Bwana:
“Ikiwa mbingu zilizo juu zitaweza kupimika
na misingi ya dunia chini
ikaweza kuchunguzwa,
ndipo nitakapowakataa wazao wote wa Israeli
kwa sababu ya yote waliyoyatenda,”
asema Bwana. 38“Siku zinakuja,” asema Bwana, “wakati mji huu utajengwa upya kwa ajili yangu, kuanzia mnara wa Hananeli hadi Lango la Pembeni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.