Yeremia 31:32
Jeremiah 31:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Halitafanana na agano nililofanya na baba zao wakati nilipowashika mkono kuwaongoza watoke Misri, kwa sababu walivunja agano langu, ijapokuwa nilikuwa mume kwao,” asema Bwana.
Jeremiah 31:32 in English
Jeremiah 31:32 · Berean Standard Bible
It will not be like the covenant I made with their fathers when I took them by the hand to lead them out of the land of Egypt— a covenant they broke, though I was a husband to them,*” declares the LORD.
Context
30Badala yake, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe; yeyote alaye zabibu chachu, meno yake mwenyewe yatatiwa ganzi. 31“Siku zinakuja,” asema Bwana,
“nitakapofanya agano jipya
na nyumba ya Israeli
na nyumba ya Yuda. 32Halitafanana na agano
nililofanya na baba zao
wakati nilipowashika mkono
kuwaongoza watoke Misri,
kwa sababu walivunja agano langu,
ijapokuwa nilikuwa mume kwao,”
asema Bwana. 33“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli
baada ya siku zile,” asema Bwana.
“Nitaweka sheria yangu katika nia zao,
na kuiandika mioyoni mwao.
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu. 34Mtu hatamfundisha tena jirani yake,
wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’
kwa sababu wote watanijua mimi,
tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,”
asema Bwana.
“Kwa sababu nitasamehe uovu wao,
wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.