Yeremia 31:15
Jeremiah 31:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo asemalo Bwana: “Sauti imesikika huko Rama, maombolezo na kilio kikubwa, Raheli akiwalilia watoto wake na anakataa kufarijiwa, kwa sababu watoto wake hawako tena.”
Jeremiah 31:15 in English
Jeremiah 31:15 · Berean Standard Bible
This is what the LORD says: “A voice is heard in Ramah, mourning and great weeping, Rachel weeping for her children, and refusing to be comforted, because they are no more.”*
Context
13Kisha wanawali watacheza na kufurahi,
vijana waume na wazee pia.
Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha,
nitawapa faraja na furaha badala ya huzuni. 14Nitawashibisha makuhani kwa wingi,
nao watu wangu watajazwa kwa ukarimu wangu,”
asema Bwana. 15Hili ndilo asemalo Bwana:
“Sauti imesikika huko Rama,
maombolezo na kilio kikubwa,
Raheli akiwalilia watoto wake
na anakataa kufarijiwa,
kwa sababu watoto wake hawako tena.” 16Hili ndilo asemalo Bwana:
“Izuie sauti yako kulia,
na macho yako yasitoe machozi,
kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,”
asema Bwana.
“Watarudi kutoka nchi ya adui. 17Kwa hiyo kuna tumaini kwa siku zijazo,”
asema Bwana.
“Watoto wako watarudi nchi yao yenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.