Yeremia 30:13
Jeremiah 30:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakuna yeyote wa kukutetea shauri lako, hakuna dawa ya kidonda chako, wewe hutapona.
Jeremiah 30:13 in English
Jeremiah 30:13 · Berean Standard Bible
There is no one to plead your cause, no remedy for your sores, no recovery for you.
Context
11Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’
asema Bwana.
‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote
ambamo miongoni mwao nimewatawanya,
sitawaangamiza ninyi kabisa.
Nitawaadhibu, lakini kwa haki.
Sitawaacha kabisa bila adhabu.’ 12“Hili ndilo asemalo Bwana:
“ ‘Kidonda chako hakina dawa,
jeraha lako haliponyeki. 13Hakuna yeyote wa kukutetea shauri lako,
hakuna dawa ya kidonda chako,
wewe hutapona. 14Wale walioungana nawe wote wamekusahau,
hawajali chochote kukuhusu wewe.
Nimekupiga kama vile adui angelifanya,
na kukuadhibu kama vile mtu mkatili angelifanya,
kwa sababu hatia yako ni kubwa mno
na dhambi zako ni nyingi sana. 15Kwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako,
yale maumivu yako yasiyoponyeka?
Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyingi
nimekufanyia mambo haya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.