Yeremia 3:23
Jeremiah 3:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilima na milimani ni udanganyifu; hakika katika Bwana, Mungu wetu, uko wokovu wa Israeli.
Jeremiah 3:23 in English
Jeremiah 3:23 · Berean Standard Bible
Surely deception comes from the hills, and commotion from the mountains. Surely the salvation of Israel is in the LORD our God.
Context
21Kilio kinasikika juu ya miinuko iliyo kame,
kulia na kuomboleza kwa watu wa Israeli,
kwa sababu wamepotoka katika njia zao
na wamemsahau Bwana Mungu wao. 22“Rudini, enyi watu msio waaminifu,
nami nitawaponya ukengeufu wenu.”
“Naam, tutakuja kwako,
kwa maana wewe ni Bwana Mungu wetu. 23Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilima
na milimani ni udanganyifu;
hakika katika Bwana, Mungu wetu,
uko wokovu wa Israeli. 24Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala
matunda ya kazi za baba zetu:
makundi yao ya kondoo na ngʼombe,
wana wao na binti zao. 25Sisi na tulale chini katika aibu yetu,
na fedheha yetu itufunike.
Tumetenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu wetu,
sisi na mababa zetu;
tangu ujana wetu hadi leo
hatukumtii Bwana Mungu wetu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.