Yeremia 25:2
Jeremiah 25:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo nabii Yeremia akawaambia watu wote wa Yuda na wale wote waishio Yerusalemu:
Jeremiah 25:2 in English
Jeremiah 25:2 · Berean Standard Bible
So the prophet Jeremiah spoke to all the people of Judah and all the residents of Jerusalem as follows:
Context
1Neno likamjia Yeremia kuhusu watu wote wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. 2Hivyo nabii Yeremia akawaambia watu wote wa Yuda na wale wote waishio Yerusalemu: 3Kwa miaka ishirini na mitatu, kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, hadi siku hii ya leo, neno la Bwana limekuwa likinijia, nami nimesema nanyi mara kwa mara, lakini hamkusikiliza. 4Ingawa Bwana amewatuma watumishi wake wote hao manabii kwenu mara kwa mara, hamkusikiliza wala hamkujali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.