Yeremia 23:26
Jeremiah 23:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe?
Jeremiah 23:26 in English
Jeremiah 23:26 · Berean Standard Bible
How long will this continue in the hearts of these prophets who prophesy falsehood, these prophets of the delusion of their own minds?
Context
24Je, mtu yeyote aweza kujificha
mahali pa siri ili nisiweze kumwona?”
Bwana asema.
“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?”
Bwana asema. 25“Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’ 26Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe? 27Wanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau jina langu, kama baba zao walivyolisahau jina langu kwa kumwabudu Baali. 28Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.